Tashkent
From Wikipedia
Tashkent (Тошкент kwa Kiuzbeki -Toshkent-, Ташкент kwa Kirusi; maana yake ni "mji wa mawe") ni mji mkuu wa Uzbekistan. Mwaka 1999 ilikuwa na wakazi 2,142,700.
Tashkent imekuwa na makazi ya kibindadamu tangu angalau miaka 1,500. Mji ulistawi kwa biashara kwenye barabara ya hariri. Baada ya kutawaliwa na Waarabu na Wamongolia mji ulitwaliwa na Urusi mwaka 1865 ukawa makao makuu ya jimbo la Turkestan.
Baada ya mapinduzi ya kibolsheviki Tashkent ilifikishwa katika Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki ingawa mazingira yake upande wa kaskazini yakawa sehemu ya Kazakhstan. 1930 imekuwa mji mkuu wa jamhuri.
Tangu 31 Agosti 1991 mji umekuwa mji mkuu wa Uzbekistan huria.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Tashkent" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Tashkent kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |