Moroko
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: الله، الوطن،الملك (Allāh, al Waţan, al Malik = Mungu, Taifa, Mfalme) |
|||||
Wimbo wa taifa: Wimbo la Sharifa | |||||
Mji mkuu | Rabat |
||||
Mji mkubwa nchini | Casablanca | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali
Mfalme
Waziri Mkuu |
Ufalme wa kikatiba Mohammad VI Driss Jettou |
||||
Uhuru - Kutoka Ufaransa - Kutoka Hispania |
Machi 2, 1956 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
446,550 km² (ya 56) Kidogo sana |
||||
Idadi ya watu - July 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
32,725,847 (ya 36) 66.8/km² (96) |
||||
Fedha | Dirham (MAD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+0) UTC (UTC+0) |
||||
Intaneti TLD | .ma | ||||
Kodi ya simu | +212 |
||||
Namba zote bila Sahara ya Magharibi |
Moroko (Ufalme wa Moroko (Kiarabu: المملكة المغربية al-mamlaka al-maghribiya "ufalme wa magharibi") ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Jina la "Moroko" limetokana na mji mkuu wa kale Marakesh. Imepakana na bahari za Atlantiki na Mediteranea; barani imepakana na Algeria na Mauretania.
Maeneo ya Kihispania ya Ceuta na Melilla ni ndani ya eneo la Moroko kwenye pwani la Mediteranea.
Mpaka wa kusini haueleweki vizuri kwa sababu Moroko inadai ya kwamba Sahara ya Magharibi ni sehemu ya eneo lake hali isiyokubaliwa na jumuiya ya kimataifa tangu Moroko ilivamia Sahara ya Kusini mwaka 1975.
Contents |
[edit] Jiografia
Eneo la Moroko ni 446,550 km². Sehemu kubwa ni jangwa la Sahara. Watu walio wengi huishi kwenye sehemu za rutba karibu na pwani.
Kuna milima inayofunika maeneo makubwa. Milima ya Rif inaongozana na pwani la Mediteranea yenye mwelekeo kutoka kaskazini-magharibi kwenda kazkazini-mashariki. Milima ya Atlas iko katikati ya nchi kutoka kusini-magharibi kwenda kaskazini-mashariki.
[edit] Wakazi
Mnamo 60 % (Januari 2005) za wakazi milioni 32.7 huishi mjini. Kiasili wakazi wengi ni Waberber na Waarabu, pamoja watu wa asili ya Andalusia (Hispania) na wa Afrika kusini ya Sahara. Waberber ndio wenyeji asilia.
Kaskazini ya nchi ambayo kitovu chake ni Fes ina zaidi tabia ya Kiarabu, kusini ambayo kitovu chake ni Marakesh zaidi ya Kiberber.
Walio wengi sana (99%) ni Waislamu Wasunni, wengine Wayahudi na Wakristo.
Wayahudi waliwahi kuwa wengi kidogo lakini idadi yao imepungua katika miaka ya nyuma kutokana na uhamiaji hata kama hali yao katika taifa ni nzuri kulingana na nchi nyingine za Kiarabu. Wakristo karibu wote ni wa asili ya Kiulaya.
[edit] Miji mikubwa
Mji mkuu ni Rabat mwenye wakazi milioni 1.2. Mji mkubwa ni Casablanca (Kiarabu: الدار البيضاء dar al-baiDa = nyumba nyeupe). Miji yote miwili mikubwa ni miji ya badari.
Miji mitano mikubwa ni kama ifuatayo (namba za sensa ya 2004):
- 1. Casablanca: wakazi 2.933.684
- 2. Rabat: wakazi 1.622.860
- 3. Fes: wakazi 946.815
- 4. Marakesh: wakazi 823.154
- 5. Agadir: wakazi 678.596
[edit] Lugha
Lugha rasmi ya nchi ni Kiarabu. Waberber wengi hasa kaskazini waliacha lugha yao na kutumia Kiarabu alkini walileta maneno yao katika lahaja ya Kiarabu cha Kimaroko.
[edit] Historia
Makala: Historia ya Moroko
[edit] Moroko ya Kale
Habari za kimaandishi ya kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani ilikuwa nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale.
Kaskazini ya nchi ikawa jimbo la Kiroma la "Mauretania Tingitana". Ikaona baadaye uvamizi wa Wavandali.
[edit] Uvamizi wa Kiarabu
Karne ya saba ilileta uvamizi wa Waarabu walioteka nchi na kusababisha Waberber kuwa Waislamu polepole. Wakati wa milki ya khalifa ya Kiabasiya Idris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea. Hii ilikuwa mwanzo wa Maroko kuwa milki ya Kiislamu ya kujitawala.
[edit] Murabitun na Muwahidun
Wafalme wa Wamurabitun (Almoravi)(1073-1147) na Wamuwahidun (Almohad) (1147-1269) walieneza utawala wao hadi Afrika ya Magharibi na juu ya sehemu kubwa ya Andalusia (Hispania), hata hadi mipaka ya Misri.
Athira ya milki ya Moroko ilipungua baadaye hadi Hispania yote imerudishwa kwa watawala wakristo mwaka 1492; pia utawala kusini ya Sahara haukuendelea. Wareno wa Wahispania waliendelea kuteka miji kwenye pwani za Moroko. Utawala wa Hispania juu ya Ceuta na Melilla ni mabaki ya nyakati zile. Sehemu za nchi zilianza kujitawala bila kukubali tena mamlaka wa juu kwa mfano makabila ya Waberber milimani au miji ya Rabat na Sale iliyounda dola ndogo la Jamhuri ya Bou Regreg katika karne ya 17 BK na kujishughulisha na uharamia.
[edit] Waalawi (1666 hadi leo)
Katika karne ya 17 familia ya Waalawi walishika mamlaka wakaendelea nayo hadi leo. Waliweza kutunza uhuru wa nchi hadi mwanzo wa karne ya 20 BK. Lakini mwanzo wa karne ya 20 Ufaransa na Hispania walimlazimisha mfalme Mulay Abdelaziz kukubali mkataba uliofanya Moroko kuwa kama koloni chini ya nchi hizo mbili.
Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilidhoofisha Ufaransa pamoja na kuingia kwa wanajeshi Waamerika na Waingereza na ahadi zao za kuleta uhuru tokeo lililohamasisha wazalendo wa Maroko kupigania upya uhuru wa nchi. Baada ya vita Wafaransa walijaribu kukandamiza mwendo huo wakamwondoa Sultani Mohammed V nchini 1953. Ghasia ikaongezeka, Sultani Muhammad V akarudi nchi ikapewa uhuri mwaka 1956.
Utawala wa mwanake Hassan II kuanzia mwaka 1961 uliitwa "miaka ya risasi" kwa sababu mfalme alikataa kukubali utaratibu wa kidemokrasia. Uchaguzi zilikuwa za uwongo wapinzani wakatupwa jela au kuuawa. Hassan II alishinda majaribio mbalimbali za kumpindua. Siasa ya kushikamana na Marekani ilimsaidia mfalme kimataifa lakini baada ya mwisho wa "vita baridi" alilazimishwa na Wamarekani kulegea utawala wake.
Mtoto wake Muhamad VI akawa mfalme kijana 1999 akaanza matengenezo ya kisiasa ya wazi zaidi.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |