Burkina Faso
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Unité, Progrès, Justice (Kifaransa: Umoja, Maendeleo, Haki) | |||||
Wimbo wa taifa: Une Seule Nuit (Usiku mmoja tu) | |||||
Mji mkuu | Ouagadougou (Wagadugu) |
||||
Mji mkubwa nchini | Ouagadougou | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali
Rais
Waziri Mkuu |
Jamhuri Blaise Compaoré Paramanga Ernest Yonli |
||||
Uhuru - Tarehe |
Kutoka Ufaransa 5 Agosti, 1960 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
274,200 km² (ya 72) 0.1% |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2003 sensa - Msongamano wa watu |
13,925,313 (ya 63) 13,228,460 51/km² (119) |
||||
Fedha | Franki ya CFA (XOF ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC) (hawafuati) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .bf | ||||
Kodi ya simu | +226 |
||||
1 Namba hizi ni kadirio ya IMF kwa mwaka 2005. |
Burkina Faso ni nchi ya Afrika ya magharibi isiyo na pwani la bahari lolote. Imepakana na nchi zifuatazao: Mali upande wa kaskazini, Niger upande wa mashariki, Benin, Togo, Ghana na Côte d'Ivoire upande wa kusini. Nchi iliwahi kuwa koloni ya Ufaransa. Tangu uhuru mwaka 1960 hadi 1984 nchi iliitwa "Volta ya Juu" (la Haute-Volta).
Contents |
[edit] Jiografia
[edit] Eneo
Eneo la Burkina Faso liko kwa kimo cha wastani ya 400 m juu ya UB. Hakuna tofauti kubwa sana. Mlima wa juu ni Ténakourou katika kusini yenye 749m. Sehemu ya chini ni bonde la mto Pendjari mpakani na Benin. Nchi iko kusini ya pinde la mto Niger
[edit] Mito na maziwa
Burkina Faso ina chanzo cha mito asilia ya mto Volta ambayo ni Mouhoun (pia Volta Nyeusi), Nakambé (pia Volta Nyeupe) na Nazinon (pia Volta Nyekundu). Mouhoun ni mto wa pekee mwenye maji mwaka wote.
Sehemu za kazkazini na mashariki za nchi ambazo ni takriban robo ya eneo lake ni beseni ya mto Niger. Tawimito ya Niger (Béli, Gorouol, Goudébo na Dargol) zina maji kwa muda wa miezi 4-6 kila mwaka.
Kuna pia maziwa kadhaa hasa Tingrela, Bam na Dem.
[edit] Hali ya hewa
Hali ya hewa ni ya kitropiki. Majira ya mvua ni kati ya Mei hadi Septemba. Wakati wa kiangazi kuna upepo wa Harmattan unaotoka katika jangwa la Sahara.
Kuna kanda tatu ya hali ya hewa, kuanzia Sahel katika kaskazini hadi Sudan-Guinea katika kusini penye mvua zaidi. Katika maeneo yabisi ya kaskazini serikali mbalimbali zimejitahidi kupanda miti, jumla ya milioni 23 katika miaka ya 1996-2000.
[edit] Wakazi
Idadi kubwa sana ya wananchi hukaa mashambani. Lakini miji inmakua haraka. Mji mkuu wa Wagadugu umeshapita idadi ya wakazi milioni moja. Wakazi wa nchi huitwa "Burkinabes" kutokana na jina la Burkina.
Miji mingine muhimu ni Bobo-Dioulasso (wakazi 366,383), Koudougou (wakazi 89.374), Ouahigouya (wakazi 62.325) na Banfora (wakazi 61.762). (namba za Januari 2006)
Kikundi kikubwa nchini ni Wamossi (nusu ya wananchi wote) wakikaa karibu na Wagadugu. Kikundi cha pili ni Wabobo (Wabwa) hasa katika eneo la Bobo-Dioulasso. Kanda la Sahel katika kaskazini wako Wapeul (Wafulani).
Lugha ya Kifaransa ni lugha rasmi. Lugha kuu za mawasiliano ni Kimossi na Kidiula.
[edit] Historia ya Burkina Faso
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |