Ardhi
From Wikipedia
Ardhi au Dunia ni mojawapo ya sayari zinazotembea katika anga ya ulimwengu. Kuna sayari tisa zinazolizunguka jua, ardhi ikiwa sayari ya tatu katika mfumo wa jua na sayari zake. Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au maili milioni 93.2. Ardhi huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake. Ardhi ina upana wa kilomita 12,756 (maili 7,973) na uzito wa kilogramu 5.97e24
Sura ya dunia au eneo la ardhi yote ni 510,066,000 kilomita mraba, ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la 148,647,000 kilomita mraba na maji yamechukuwa eneo la 361,419,000 kilomita mraba. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu 148,647,000 kilomita mraba ni asilimia 29.1.
Kati ya maeneo yaliyofunikwa na maji ni bahari yanayofunika eneo la 335,258,000 kilomita mraba ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ya maziwa, mabwaba na mitoni ni asilimia 3 tu.
Contents |
[edit] Muundo wa dunia
- - taz. makala "Muundo wa dunia" -
Muundo wa dunia yetu ni ya tabaka mbalimbali zinazofuatana kutoka nje kwenda ndani. Kila moja ina tabia yake.
Tabaka | Kuanzia kilomita |
---|---|
Ganda la nje | 0 - 40 |
Koti ya juu | 40 - 400 |
Koti ya kati | 400 - 900 |
Koti ya chini | 650 - 2900 |
Kiini cha nje | 2900 - 5100 |
Kiini cha ndani | 5100-6371 |
Kila ukiingia ndani ardhi inazidi kuwa moto mpaka ukifika ndani kabisa daraja ya harara hufikia nyuzi 5000-6000°C.
[edit] Hewa ya ardhi
Ardhi ni sayari pekee mpaka sasa ambayo binadamu na viumbe vyengine vya ardhini vinaweza kuishi na hii ni kwa sababu hewa yake ni ya namna ya pekee. Kuna katika hewa ya ardhi asilimia 78 ya naitrojini, asilimia 21 ya oksijini na asilimia 1 ya aina nyenginezo za hewa, na kwa sababu hii uhai na maisha yanamakinika katika ardhi, kinyume na sayari nyenginezo.
[edit] Kuumbwa kwa ardhi
Kabla ya kuumbwa kwa ardhi, mbingu zote na ardhi zilikuwa kitu kimoja kilichoambatana kisha Mwenyezi Mungu akavitatanua na kusababisha mlipuko mkubwa kabisa ambao ulitawanya na kupeperusha kila kitu katika anga, na haya yanakubaliana na nadharia ya sayansi leo inayosema kuwa ulimwengu ulianza na mlipuko mkubwa.
[edit] Kuhusu ardhi
Sehemu kubwa kabisa ya ardhi inafunikwa na bahari, kwani takriban asilimia 70 ya ardhi inafunikwa na maji ya bahari na kutokana na maji yote yaliyokuwepo ardhini, asilimia 97 ni maji ya bahari, na asilimia 3 ni maji matamu.
Bahari Kuu | Eneo lake | Kina chake |
---|---|---|
Pasifiki | maili 64,186,000 muraba | futi 15,215 |
Atlantiki | maili 33,420,000 muraba | futi 12,881 |
Bahari Hindi | maili 28,350,000 muraba | futi 13,002 |
Bahari ya Antaktika | maili 7,848,300 muraba | futi 13,100 - 16,400 |
Bahari ya Aktika | maili 5,106,000 muraba | futi 3,953 |
[edit] Juu ya ardhi
Hewa iliyoko juu ya ardhi vile vile ina tabaka saba, na kila tabaka ina kazi yake. Hewa kwa jumla ina masafa ya kiasi cha kilomita 560 au maili 348 kuendea juu, na baada ya hapo unaingia kwenye anga za juu. Hewa hii ndio inayotukinga sisi viumbe na madhara ya jua na vitu vyenginevyo ambavyo vinaingia anga la dunia na kuteremka ndani ya ardhi.
Mfumo wa jua na sayari zake |
---|
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Meriki - Mshtarii - Zohari - Uranus - Neptun |