Umoja wa Kisovyeti
From Wikipedia
Umoja wa Kisovyeti (Советский Союз, sovjetskii soyuz, kifupi cha: Umoja wa Jamhuri za Kisovyeti za Kijamii) ilikuwa nchi kubwa duniani kati ya 1922 hadi 1991. Ilianzishwa katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 ikachukua nafasi ya Dola la Urusi la awali. Umoja wa Kisovyeti ulitawaliwa na chama cha kikomunisti. Wakomunisti waliamua kutawala Dola la Urusi la awali kwa muundo wa shirikisho wakaunda jamhuri mbalimbali kufuatana na mataifa ndani ya eneo hili kubwa.
Kikatiba jamhuri hizi zote zilikuwa nchi huria lakini hali halisi zilitawaliwa zote kutoka makao makuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Katiba ilipata umuhimu tangu 1989 wakati wa mwisho wa utawala wa Wakomunisti ambako jamhuri zote zilitafuta uhuru wao zikaachana na Umoja.
Mwaka 1991 jamhuri wanachama za mwisho Urusi, Belarus na Ukraine ziliamua kumaliza Umoja wa Kisovyeti.
Contents |
[edit] Viongozi
[edit] Makatibu Wakuu wa Chama cha Kikomunisti
- Vladimir Lenin
- Josef Stalin
- Nikita Krushchov
- Leonid Brezhnyev
- Yuriy Andropov
- Konstantin Chernenko
- Mikhail Gorbachov
[edit] Jamhuri za Umoja wa Kisovyeti
[edit] Jamhuri za Kisovyeti (zote zimekuwa nchi huria)
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiarmenia imekuwa Armenia
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiazeri imekuwa Azerbaijan
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kibelarus imekuwa Belarus
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiestonia imekuwa Estonia
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kigeorgia imekuwa Georgia
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi imekuwa Kazakhstan
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikirgizi imekuwa Kirgizia
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kilatvia imekuwa Latvia
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kilithuania imekuwa Lithuania
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova imekuwa Moldova
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kirusi imekuwa Urusi
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kitajiki imekuwa Tajikistan
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kizturkmeni imekuwa Turkmenistan
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine imekuwa Ukraine
- Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki imekuwa Uzbekistan