Nikaragua
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Pro Mundi Beneficio (Kilatini: Kwa salama ya dunia) |
|||||
Wimbo wa taifa: Salve a ti, Nicaragua (Usalimiwe Nikaragua) |
|||||
![]() |
|||||
Mji mkuu | Managua |
||||
Mji mkubwa nchini | Managua | ||||
Lugha rasmi | Kihispania (kitaifa) (Kiingereza lugha za kieneyeji kimahali kwenye pwani la Karibi) | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri Enrique Bolaños |
||||
Uhuru Imetangazwa Imetambuliwa |
15 Septemba 1821 25 Julai 1850 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
130,000 km² (ya 97) 14.01 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
5,487,000 (ya 108) 42/km² (ya 157) |
||||
Fedha | Cordoba (NIO ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-6) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .ni | ||||
Kodi ya simu | +505 |
Nikaragua ni nchi ya Amerika ya Kati yenye wakazi milioni 5.5. Imepakana na Honduras na Kosta Rika; upande wa magharibi ni pwani la Pasifiki na upande wa mashariki kuna pwani la Bahari ya Karibi.
Jina la nchi linasemekana kuwa mchanganyiko wa jina la wakazi asilia walioitwa "Nikarao" na neno la Kihispania la "agua" (=maji) kutokana na maziwa makubwa mawili nchini yanayoitwa Lago Managua na Lago Nicaragua. Maelezo mengine yanamtaja chifu wa wazalendo wakati wa kufika kwa Wahispania aliyeitwa "Nikarao".
Contents |
[edit] Wakazi
Wakazi walio wengi sana hukalia maeneo ya mji mkuu Managua na pwani la Pasifiki. Sehemu kubwa (70 %) ni chotara kati ya wakazi asilia na Wazungu. Takriban asilimia 10 za Wanikaragua ni wa asili ya kiafrika wakikaa hasa kwenye pwani la Bahari ya Karibi.
[edit] Jiografia
Nikaragua ina volkeno nyingi; nyororo ya milima ya kivolkeno hufuata mstari wa pwani la Pasifiki. Sehemu ya juu ni mlima Mogoton mwenye kimo cha 2,438 m juu ya UB. Maziwa makubwa mawili ya maji matamu ni Lago Managua na Lago Nicaragua. Eneo upande wa Karibi ina wakazi wachache sana ni hasa eneo la misitu minene.
[edit] Historia
Nchi ilikuwa koloni ya Hispania tangu 1524. Mwaka 1821 iliachana na utawala wa Hispania pamoja na nchi jirani na kuingia katika Shirikisho la Amerika ya Kati. Tangu mwaka 1854 imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.
[edit] Viungo vya Nje
[www.pronicargua.org.ni]
[edit] Sanaa na utamaduni
- Nicaraguan Art Art and Literature by Nicaraguans
- Ruben Dario