Visiwa vya mfereji wa Kiingereza
From Wikipedia
Visiwa vya Mfereji wa Kiingereza ni funguvisiwa ya visiwa tisa katika Mfereji wa Kiingereza karibu na pwani la Ufaransa vyenye wakazi 160,000.
Visiwa vitano vikubwa ni:
- Jersey
- Guernsey
- Alderney
- Sark
- Herm
Kiutawala vimegawiwa kwa sehemu mbili: eneo la Jersey na eneo la Guernsey lakini visiwa kadhaa vina kiasi kikubwa cha uhuru pekee vyao.
[edit] Hali ya kisiasa
Visiwa hivi vina hali ya pekee. Vyote ni "maeneo chini ya taji la Uingereza" lakini si sehemu za Ufalme wa Maungano au Uingereza mwenyewe. Havishiriki katika bunge la London wala havipaswi kupokea sheria za bunge hili bali vina bunge zao za Jersey, Guernsey, Alderney na Sark pamoja na watendaji na mahakama. Mfalme au malkia wa Uingereza ana wajibu wa kutetea visiwa na kushughulika mambo ya nje. Hali halisi wajibu hizi zinangaliwa na serikali ya Uingereza kwa niaba ya malkia.
Madaraka ya malkia (au: mfalme) yametokana na cheo chake cha kale kama Mtemi Mkuu wa Normandy miaka 800 iliyopita. Kihistoria visiwa vilikuwa sehemu ya Normandy na mwaka 1066 mtemi wa Normandy alishambulia na kuteka Uingereza. Kuanzia sasa wafuasi wake waliendelea na vyeo viwili vya Mfalme wa Uingereza na Mtemi wa Normandy na hivyo mkuu wa visiwa. Katika karne iliyofuata wafalme wa Ufaransa walitwaa Normandy lakini walishindwa kuteka viwia vidogo. Hali ya visiwa haikubadilishwa kisheria havikuunganishwa na ufalme wa Uingereza hivyo hadi leo ni mabaki madogo ya mali ya wafalme wa Uingereza katika Ufaransa wa leo.
Hivyo visiwa si sehemu za Uingereza wala sehemu za Umoja wa Ulaya viko ndani ya ushuru wa pamoja wa Ulaya lakini vina haki ya kuongeza kodi zao.
Mwakilishi wa malkia yaani serikali ya Uingereza ni Gavana.
[edit] Uchumi
Uchumi wa visiwa umetegemea hasa utalii, huduma za benki na kilimo. e tourism, horticulture (growing plants for food) and financial services (businesses to do with money). Most people speak English, although some people in Guernsey, Jersey and Sark still speak the traditional language of their island.
[edit] Utamaduni
Visiwa vyote vilikuwa na lugha zao ambazo ni aina za Kinormandy kinachozungumzwa pia kama lugha ya kieneo Ufaransa bara. Idadi ya wasemaji imepungua kuna hasa maelfu kadhaa Guernsey na Jersey. Lugha rtasmi kwa shughuli za serikali ni hasa Kiingereza lakini pia Kifaransa.
Nchi na maeneo ya Ulaya | |
---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Eire | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Italia | Jamhuri ya Masedonia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Malta | Moldova | Monako |Montenegro | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikani
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro |