Dinosau
From Wikipedia
Dinosau ni wanyama jamii ya mijusi walioishi miaka mamilioni iliyopita katika kipindi kilichojulikana kama Zama za Mesozoic. Dinosau wakubwa wana urefu wa futi 100 na 50 hivi na wale wadogo zaidi wana ukubwa kama wa kuku hivi. Historia ya maisha yao hasa kuzaliana ni ngumu kidogo kwani kwa mfano ukichukua masalia yao huwezi kujua yupi jike na yupi dume. Wengi walitembea kwa miguu miwili na wengine minne, wako waliokuwa na pembe na ngozi yao ngumu misili ya ile ya tembo. Hii ilikuwa ni miaka milioni 165 iliyopita kwenye kipindi cha Zama za Mesozoic kipindi hiki ambacho dunia ilikuwa haijagawanyika katika mabara kama ilivyo hivi sasa ilikuwa ikiitwa Pangaea.
Makala hiyo kuhusu "Dinosau" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Dinosau kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |