Pi
From Wikipedia
Pi ni herufi ya kumi na sita Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama Π (herufi kubwa cha mwanzo) au π (herufi ndogo ya kawaida).
Katika Ugiriki ya Kale ilihesabiwa pia kama namba "80".
Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fisikia. Imejulikana hasa kama namba ya duara kwa thamani ya 3.14159. 22/7 ni karibu zaidi na Pi na 355/113 ni karibu zaidi.