Zohari
From Wikipedia
Zohari ni sayari ya sita toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake. Ni sayari kubwa ya pili baada ya Mshtarii.
Inaonekana kwa macho matupu si lazima kutumia darubini. Kwa hiyo imeshajulikana tangu zamani ilitambuliwa na wataalamu wa nyakati za kale.
Inazunguka jua katika muda wa miaka ya dunia 29 na siku 166.
Uso wa Zohari haionekani kwa sababu angahewa nzito inafunika kila sehemu. Mada ya angahewa ni hasa hidrojeni. Kutokana na uzito wa angahewa shindikizo ndani yake inaongezeka sana katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili (majimaji) inayobadilika kuwa mango (imara) hadi metali ndani zaidi.
[edit] Miezi ya Zohari
Zohari ina miezi mingi. Miezi thelathini imepewa majina. Kati ya miezi hii Titan ni mkubwa mwenye kipenyo cha 5,150 km. Ni mwezi wa pekee unaojulikana kuwa na angahewa. Miezi ya Rhea, Dione, Tethys na Iapetus ina vipenyo kati ya 1,050 km na 1,530 km.
[edit] Bangili za Zohari
Tabia ya pekee ya Zohari ni bangili zake. Mtu wa kwanza wa kuziona alikuwa Galileo Galilei alipolenga darubini yake kwa sayari. Lakini Galilei alishindwa kutmabua alichoona kutokana na kasoro za darubini yake. Aliandika wakati ule ya kwamba Zohari ilikuwa na "masikio". Mwaka 1655 Mholanzi Christiaan Huygens aliweza kutumia darubini kubwa zaidi akatambua masikio ya Galilei kuwa bangili inayozunguka sayari.
Siku hizi imejulikana ya kwamba bangili ni vipande vya barafu, vumbi ba mawe. Vipande vyake vina ukubwa kati ya milimita chache hadi mita kadhaa kama motokaa. Unene wa bangili ni mita mamia kadhaa.
Makala hiyo kuhusu "Zohari" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Zohari kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Mfumo wa jua na sayari zake |
---|
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Meriki - Mshtarii - Zohari - Uranus - Neptun |