Baghdad
From Wikipedia
Baghdad (Kar.: بغداد ) ni mji mkuu pia mji mkubwa nchini Iraq. Iko kando la mto Tigris.
Baghdad iliundwa na Waarabu badala ya mji mkuu wa kale Ktesiphon katika karne ya 8. Ilikuwa mji mkuu wa dunia ya Uislamu wakati wa ukhalifa wa Abbasiyya. Mwaka 1258 mji uliharibiwa na jeshi la Mongolia.
Baadaye ilikuwa makao makuu ya utawala wa Mesopotamia katika Dola la Uturuki. Tangu 1921 ilitawaliwa na Uingereza pamoja na Iraq yote. Tangu 1936 ilikua mji mkuu wa Iraq kama nchi ya kujitegemea.
Mji uliharibiwa na Vita ya Ghuba na vita ya wenyewe kwa wenywe nchini Iraq.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Baghdad" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Baghdad kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |