Sumeri
From Wikipedia
Sumeri ilikuwa kati ya tamaduni za kwanza za juu katika Asia ya Magharibi na hasa Mesopotamia (Iraq ya leo). Labda ilikuwa utamaduni wa kwanza wa kujenga miji.
Sumeri ilianzishwa na kuendelea kwenye nchi yenye rutba kati ya mito Frati na Hidekeli tangu mwaka 3,500 KK. Elimu ya akiolojia iliweza kuthebitisha ya kwamba Wasumeri walijenga miji na kuendeleza maandishi. Maandishi yao yamehifadhiwa kwa sababu waliandika mengi kwa kuchora maneno kwenye vipande vya udongo wa ufinyanzi na kuvichoma. Imetambuliwa pia ya kwamba waliweka misingi muhimu kwa kalenda za leo kwa kugawa siku katika masaa 24 na saa katika dakika 60.
Wasumeri waliishi katika dola-miji iliyotawaliwa na wafalme au makuhani.
Makala hiyo kuhusu "Sumeri" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Sumeri kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |