Saint Helena
From Wikipedia
Lugha rasmi | Kiingereza |
Mji Mkuu | Jamestown |
Serikali | Eneo la ng'ambo la Uingereza |
Mkuu wa Dola | Elisabeth II |
Gavana | Michael Clancy |
Eneo (pamoja na visiwa vya pembeni) | 414 km² |
Idadi ya Wakazi | 7460 (Julai 2005) |
Wakazi/km² | 18 |
Pesa | Pauni ya St. Helena |
Saa za eneo | UTC |
Wimbo la Taifa | God Save the Queen |
Saint Helena (Kiingereza: Mtakatifu Helena) ni kisiwa mbele ya Afrika ya Magharibi katika Atlantiki ya kusini chenye eneo la 122 km². Umbali na Angola ni 1.868 km, ni 3.290 km hadi Brazil (Amerika ya Kusini). Kisiwa chenye asili ya kivolkeno kimo ndani ya beseni ya Angola ya bahari Atlantiki hivyo huhesabiwa kuwa kisiwa cha Afrika. Ni eneo la ng'ambo la Uingereza na makao makuu ya kundi la visiwa vidogo pamoja na kisiwa cha Ascension na funguvisiwa ya Tristan da Cunha.
[edit] Historia ya Wakazi
Wakazi 7.460 (Julai 2005) ni wa asili ya Kiulaya, Kiafrika na Kichina. Wote wana uraia wa Uingereza wakitumia ligha ya Kiingereza.
Kihistoria Saint Helena haikuwahi kuwa na wakazi kabla ya kufika kwa Wareno mwaka 1502 BK waliojenga nyumba za kwanza bila kuacha wakazi wa kudumu. Katika miaka iliyofuata palikuwa na mavutano kati ya Wareno, Waholanzi na Waingereza.
Tangu 1673 Kampuni ya Kiingereza ya India ya Mashariki ilitawala kisiwa kama kituo cha safari za merikebu ya matanga kubwa kati ya Uningereza, Afrika ya Kusini na India. Kampuni ilianzisha mji wa Jamestown na mashamba makubwa ya mboga kwa ajili ya mabaharia waliopita. Kwa ajili ya watumwa Waafrika walipelekwa Saint Helena, baada ya mwisho wa utumwa katika karne ya 19 pia wafanyakazi Wachina.
[edit] Napoleon
Jina la Saint Helena lilijulikana kote duniani kutokana na kuwa mahali pa kufungwa kwa Kaisari Napoleon I. wa Ufaransa. Napoleon alikuwa kiongozi aliyeogopwa sana na kutawala sehemu kubwa ya Ulaya kwa miaka kadhaa mwanzoni wa karne ya 19. Baada ya kushindwa mwaka 1814 alitakiwa kubaki kwenye kisiwa cha Elba (Italia) alipotoroka tena na kuanza vita upya. Baada ya kushindwa mara ya pili huko Waterloo Waingereza walimpeleka mahali pa mbali iwezekanavyo ndipo St. Helena mwaka 1815. Hapo aliishi katika hali ya kufungwa akiwa na nyumba yake na watumishi wake lakini alipaswa kuongozana kisiwani na maafisa Waingereza waliomfuata kila alikoenda. Kwa ujumla Waingereza walipeleka St. Helena wanajeshi 2,000 pamoja na mabaharia wa kijeshi 500 ili wamlinde Napoleon wakiogopa majaribio ya Wafaransa kumwondoa na kumrudisha katika hali ya uhuru.
Napoleon alikufa mwaka 1821 akazikwa kisiwani lakini mwili wake ulihamishwa baadaye kwenda Ufaransa alikopewa kaburi la heshimi Paris mjini. Ufaransa ilinunua baadaye nyumba alimoishi kutoka Uingereza ni mahali pa kumbukumbu pa kitaifa pa Ufaransa hadi leo.
[edit] Hali ya St. Helena leo
Kisiwa kinafikiwa kwa meli tu haina kiwanja cha ndege kubwa. Lakini hakuna meli za tanga tena zinazohitaji kusimama St. Helena na kuchukua maji pamoja na chakula. Hivyo hali ya uchumi ni duni. Kuna uvuwi kidogo na utalii unaotegemea kumbukumbu ya Napoleon. Kuna meli moja tu ya kuhudumia St. Helena na visiwa vingine inafika taktiban mara mbili kwa mwezi. Muda wa safari kati ya St. Helena na Namibia au Afrika Kusini ni siku 4 au 5. Kwa ujumla kisiwa kinategemea misaada ya serikali ya Uingereza.
Mji mkuu ni Jamestown mwenye wakazi 900.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |