Eritrea
From Wikipedia
|
|||||
Hadabu ya Taifa: Nie nie | |||||
![]() |
|||||
Lugha za Taifa | Tigrinya, Kiarabu na Kiingereza |
||||
Mji Mkuu | Asmara | ||||
Rais | Isaias Afewerki | ||||
Eneo - Total - % Maji |
Kadiriwa 97th 121,320 km² Acha |
||||
Idadi ya Watu - Makadirio (2005) - Jumla (2002) - Chumo cha Umma kugawa na Eneo |
Kadiriwa 115th 4,561,599 4,298,269 38/km² (135th) |
||||
GDP (PPP) - Jumla - Kwa Kila Raia (Per capita) |
2005 estimate 4,250 (155th) 917 (177th) |
||||
Uhuru - Kadirifu - Barabara |
Kutoka Ethiopia (Uhebeshi) Mai 29, 1991 Mai 24, 1993 |
||||
Fedha | Nakfa | ||||
Saa za Eneo | UTC +3 | ||||
Wimbo wa Taifa | Ertra, Ertra, Ertra | ||||
Intaneti TLD | .er | ||||
Kodi ya simu | 291 |
Eritrea ni nchi ya Afrika kaskazini-mashariki. Eneo hili hujulikana pia kama Pembe ya Afrika. Upande wa Magharibi imepakana na Sudan, upande wa Kusini imepakana na Ethiopia, na Kusini-Mashariki kuna nchi ya Djibouti. Mashariki na Kusini-Mashariki Eritrea ina pwani ndefu ya Bahari ya Shamu.
Jina la nchi limeanzishwa mnamo mwaka 1890 na wakoloni Waitalia kutokana na neno la Kigiriki "erythraîa" linalomaanisha “bahari nyekundu”. Hii ni kwa sababu Bahari ya Shamu iliitwa "Sinus Erythraeus" na mabaharia Wagiriki au “Mare Erythraeum” kwa kilatini na Waroma wa kale – maana yake ni "bahari nyekundu" – tazama Kiingereza “Red Sea”.
Contents |
[edit] Historia
Angalia makala: Historia ya Eritrea
Historia ya Eritrea kama eneo la pekee jinsi ilivyopata uhuru mwisho wa karne ya 2o ilianza na ukoloni wa Italia. Hadi karne ya 19 maeneo ya Eritrea yalikuwa sehemu ya Ethiopia. Pwani lilikaa karne nyingi chini ya utawala wa Uturuki au baadaye Misri kama nchi zenye nguvu kwenye Bahari ya Shamu.
[edit] Koloni ya Italia
1869 kampuni ya Kiitalia ilinunua bandari ya Assab iilyokuwa koloni ya serikali ya Italia 1882. Italia ilipanusha utawala wake kwa kutwaa mji wa Massawa 1885 na kuchukua pia pwani lote kati ya miji miwili. Baadaye Waitalia walianza kuelekea nyanda za juu na Ethiopia yote. Mwendo huu ulisimamishwa na Ethiopia katika mapigano ya Adowa mwaka 1896. Italia ilikubali uhuru wa Ethiopia na Ethiopia ilikubali koloni ya Italia katika Eritrea.
Koloni ilianzishwa rasmi mwaka 1890 kwa jina la "Eritrea" kutokana jina la kale ya "Mare Erytraeum" au Bahari ya Eritrea.
Utawala wa Italia ilileta mabadiliko mengi kati ya watu wa koloni na kujenga jamii mpya na tofauti na wakazi wa Ethiopia hivyo kuweka msingi wa taifa la pekee. Tangu mwaka 1922 serikali mpya ya Italia ya Mussolini ilianzisha siasa ya ubaguzi wa rangi na kuwatendea wenyeji kwa dharau.
Kuanzia 1935 Eritrea ilikuwa mahali pa kuanzisha vita mpya ya Italia dhidi ya Ethiopia.
[edit] Eneo lindwa la Uingereza
Katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia jeshi la Italia katika Ethiopia ilishindwa na Waingereza na Ertitrea kutawaliwa tangu 1941 na Uingereza. 1952 Eritrea ilikabidhiwa na Umoja wa Mataifa kwa Ethiopia kama eneo la pekee.
[edit] Chini ya Ethiopia
Serikali ya Haile Selassie ililenga kuunganisha Eritrea tena na Ethiopia na kwa mbinu mbalimabli ilipata kura ya bunge la Eritrea ya kujivunja na kuwa jimbo la Ethiopia.
Baada ya tukio hili vikundi vya wanamigambo walienda porini kupigania kwa silaha uhuru ya Eritrea. Baada ya vita ya miaka 30 harakati ya Eritrean People's Liberation Front (EPLF) ilishinda jeshi la Ethiopia mwaka 1991. Usindi huu ulikuwa baadaya sababu kuu ya kuanguka kwa serikali ya kikomunisti ya Ethiopia.
[edit] Eritrea huru
Baada kura ya wakazi wa Eritrea uhuru wa nchi ilitangazwa tarehe 24 Mei 1993. Awali uhusiano na serikali mpya ya Ethiopia ulikuwa mzuri lakini baada ya miaka ya kwanza ulianza kuzorota.
1998 kulitokea vita kati ya Eritrea na Ethiopia uliokwisha na ushindi wa Ethiopia. Wanajeshi la kulinda amani ya UM wanajaribu kutunza hali ya kutopigana.
[edit] Siasa
- Kifungu chenye we: Siasa za Eritrea
Bunge la Taifa la viti 150, iliyo tekezwa mwaka 1993 baada ya Uhuru, Bunge hiyo ilimchagua Rais wa sasa, Isaias Afewerki. Kura za Nchi huwa zinapagwa na kupanguliwa. Shina za taarifa madaraka za kutangaza habari kwa siasa za nyumbani Eritrea haziko; na September 2001 serikali ilifunga wataarifi midia zakibinafsi, na watu wanaopinga serikali kufugwa bila kushtakiwa, hii yote ni kutoka taarifa ya washufu wa ulimwengu, kama Waangalizi wa haki za Kibinadamu (Human Rights Watch) and Wakobozi wa Kimataifa (Amnesty International). Mwaka wa 2004 Idara ya jimbo za marekani (U.S. State Department) iliamua kwamba Eritrea ni Nchi maksusi Kujalisha (Country of Particular Concern, au CPC) ya kufinyilia Dini (Ona chini hapa).
Mambo ya inje yanahusu vita na Ethiopia na Sudan. Baada ya wajumbe wa serikali ya Eritrea wa Idara ya mambo za kigeni kuenda Sudani, ushirikiano umeanza kuwa wakawaida. Bishano na Ethiopia bado ni mawazo makubwa ya chuki abayo imemfanya Rais kuiambia Muungano wa Kimataifa UN ichukua hatua. Uagizaji huu umelezwa kwa barua kumi na moja uadishi wa Rais[1].
[edit] Eneo
- Kifungu chenyewe: Eneo za Eritrea
Eritrea Mgao Eneo 6:
- Kati (Maekel)
- Anseba
- Kisini ziwa lekundu (Debubawi-Keih-Bahri)
- Kaskazini ziwa lekundu (Semienawi-Keih-Bahri)
- Kusini (Debub)
- Gash-Barka
[edit] Jiografia
- Kifungu chenyewe: Jiografia ya Eritrea
Eritrea iko kwa eneo la Pembe la Afrika na imepakana na Bahari ya Shamu kaskazini mashariki. Kwa mchanga wa pwani uliyo Eneo Kame pahali pa kutega samaki ni Dahlak Achipelago. Eneo ambayo iko kwa milima kusini si kame vile lakini hali ya hewa ni poa. Mlima juu zaidi ni Soira, ambao huko kati ya Nchi Eritrea, 3018 m Juu ya bahari.
Mji mkuu wa Eritrea ni Asmara na miji mingine ni kama mji wa bandari Assab kusini mashariki, na pia miji kama Massawa na Keren.
[edit] Uchumi
- Kifungu chenyewe: Uchumi wa Eritrea
Nchi za Afrika | ![]() |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |